KUITWA KAZINI UTUMISHI


 

Tangazo la Kuitwa Kazini Ajira Portal 2026

Tangazo la Kuitwa Kazini 2026

Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma

Tarehe: 08 Mei 2026
Kumbukumbu: JA.9/18/01"E"/12

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza rasmi majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi katika taasisi na halmashauri mbalimbali nchini Tanzania. Tangazo hili linahusisha waombaji waliofanya usaili kati ya tarehe 25 Aprili 2025 hadi 21 Januari 2026.

Walioitwa Kazini Wanatakiwa Kufanya Nini?

Waombaji wote waliofaulu usaili wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal kupitia sehemu ya My Applications ili kupakua barua zao za ajira na kwenda kuripoti kwenye vituo walivyopangiwa.

  • Pakua barua ya ajira kupitia Ajira Portal
  • Chapisha nakala ya barua hiyo
  • Ripoti kwa mwajiri ndani ya muda uliopangwa
  • Nenda na vyeti halisi vya masomo kwa uhakiki

Kada Zilizotajwa Katika Tangazo

Kada Baadhi ya Maeneo
Walimu wa Sekondari Musoma, Bunda, Rorya, Tarime, Moshi
Walimu wa Msingi Ludewa, Moshi, Monduli, Tarime
Tabibu na Afya Musoma, Tarime, Bunda
Wahasibu Musoma, Tarime, Bunda
Maafisa Sheria Musoma, Tarime, Bunda
Maafisa Mifugo Monduli, Moshi, Tarime
Maafisa Mazingira Rorya, Bunda

Mambo Muhimu ya Kuzingatia

  • Majina yote yapo ndani ya PDF rasmi ya Ajira Portal
  • Wasioona majina yao hawakufaulu au hawakupata nafasi
  • Endelea kufuatilia matangazo mengine ya ajira
  • Ripoti kwa wakati ili kuepuka kupoteza nafasi yako

Jinsi ya Kupakua Orodha Kamili

Bonyeza link hapa chini kupakua tangazo rasmi lenye majina yote ya walioitwa kazini pamoja na vituo vyao vya kazi.

PAKUA PDF HAPA
Previous Post Next Post