TANGAZO LA KUITWA KAZINI UTUMISHI – MEI 2026
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza rasmi majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi katika taasisi mbalimbali za serikali.
Kumbukumbu Na: JA.9/18/01"E"/7
Muhtasari Muhimu wa Tangazo
Waombaji kazi waliofanya usaili kati ya tarehe 24 Aprili 2025 hadi 14 Februari 2026 wamepata matokeo yao kupitia tangazo hili. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwa kwenye kanzidata (Database) waliopangiwa kazi baada ya nafasi kupatikana.
Jinsi ya Kupata Barua ya Ajira
Waombaji wote waliofaulu wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal kisha:
- Nenda sehemu ya My Applications
- Pakua barua ya kupangiwa kazi
- Chapisha (Print) kwa matumizi ya kuripoti kazini
Masharti ya Kuripoti Kazini
- Kuripoti ndani ya muda uliotajwa kwenye barua
- Kuja na vyeti halisi (Original Certificates)
- Vyeti viwe kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea
- Vyeti vitahakikiwa kabla ya kupewa ajira rasmi
Kuhusu Wasiopata Nafasi
Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, wanashauriwa kuendelea kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa kwani hawakufaulu au hawakupata nafasi katika awamu hii.
Baadhi ya Kada Zilizotangazwa
- Afisa Maendeleo ya Michezo
- Afisa Sheria
- Wakaguzi wa Ndani
- Wasaidizi wa Afya
- Madaktari (Clinical Officers)
- Walimu wa Shule za Msingi
- Wahasibu
- Maafisa Kilimo na Mifugo
- Wahandisi na Mafundi Sanifu
Hitimisho
Hili ni fursa muhimu kwa waliofanikiwa kuitwa kazini. Hakikisha unafuata maelekezo yote kwa usahihi ili kuepuka kupoteza nafasi yako.
PAKUA PDF HAPA
