MAFASI YA KAZI UTUMISHI


 

Tangazo la Ajira Malinyi DC 2026

Ajira Mpya: Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi 2026

Kumb.Na.HA.331/388/01/04
Tarehe: 04/05/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ametangaza nafasi za ajira kwa Watanzania wenye sifa stahiki. Nafasi zilizotolewa ni 2 za Mwandishi Mwendesha Ofisi.

Majukumu ya Kazi

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
  • Kutunza kumbukumbu za miadi, vikao na safari za Mkuu wa Idara.
  • Kutafuta na kusambaza majalada kwa maofisa husika.
  • Kukusanya na kurejesha nyaraka sehemu husika.
  • Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao.
  • Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi.
  • Kufanya kazi nyingine zitakazopangwa na Mkuu wa kazi.

Sifa za Mwombaji

  • Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
  • Stashahada (Diploma ya Uhazili) au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
  • Uwezo wa kuchapa Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika.
  • Ujuzi wa programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Ngazi ya Mshahara

TGS C

Masharti ya Jumla

  • Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18–45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba.
  • Kuambatanisha CV yenye maelezo binafsi, anuani, simu na referees watatu.
  • Vyeti vya elimu na taaluma lazima vithibitishwe na Mwanasheria/Wakili.
  • Vyeti vya nje ya nchi lazima vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
  • Waombaji waliostaafu hawaruhusiwi bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Maombi ya kughushi yatapelekea hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi: 19/05/2026.

Jinsi ya Kuomba

Waombaji wanapaswa kuwasilisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu kwa anuani:

Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi,
S. L. P 18,
MALINYI.

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia Recruitment Portal.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatazingatiwa.

Previous Post Next Post