UTUMISHI: Tangazo Rasmi la Kuitwa Kazini Mei 2026
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa rasmi tangazo jipya la kuitwa kazini kwa waombaji walioshiriki usaili katika vipindi tofauti kati ya Mei 2025 hadi Desemba 2025.
Tangazo hili linahusisha waombaji waliopita usaili pamoja na baadhi ya waliokuwa kwenye kanzidata (Database) ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Mambo Muhimu Unayopaswa Kujua
- Majina ya waliofaulu yameorodheshwa rasmi kwenye tangazo hili.
- Barua za ajira zinapatikana kupitia akaunti ya Ajira Portal.
- Unatakiwa kupakua na kuchapisha barua yako kabla ya kuripoti kazini.
- Ripoti kazini ndani ya muda uliopangwa kwenye barua yako.
- Hakikisha unaenda na vyeti halisi (Original Certificates).
Kada Zilizohusika
Baadhi ya kada zilizopata nafasi katika tangazo hili ni pamoja na:
- Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari
- Afisa Maendeleo ya Michezo
- Afisa Mifugo
- Afisa Ushirika
- Msaidizi wa Afya
- Msaidizi wa Hesabu
- Tabibu (Clinical Officer)
Maelekezo Muhimu kwa Walioitwa Kazini
Waombaji wote waliofanikiwa wanapaswa:
- Kuingia kwenye akaunti yao ya Ajira Portal
- Kupakua barua ya ajira (Download & Print)
- Kuripoti kwenye kituo walichopangiwa
- Kuwasilisha vyeti halisi kwa uhakiki
Kwa Ambao Hawajafanikiwa
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi kwa awamu hii. Hata hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa.
Pakua Orodha Kamili
Ili kuona majina yote pamoja na vituo vya kazi kwa undani zaidi, bofya hapa chini:
PAKUA PDF 03
