TANGAZO LA KUITWA KAZINI PSRS Mei 2026 – Majina ya Walioitwa Kazini Halmashauri za Maswa, Busega na Itilima
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetoa rasmi tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji kazi waliofaulu usaili uliofanyika kati ya tarehe 28 Mei 2025 hadi 23 Desemba 2025.
Tangazo hili linahusisha kada mbalimbali zilizopangiwa vituo vya kazi katika Halmashauri za Wilaya ya Maswa, Busega pamoja na Itilima.
Kada Zilizotajwa Kwenye Tangazo
- Afisa Maendeleo ya Michezo Daraja la II
- Afisa wa Sheria Daraja la II
- Mhasibu Daraja la II
- Msaidizi wa Afya Daraja la I
- Msaidizi wa Hesabu Daraja la II
- Mwalimu Daraja la IIIA
- Tabibu Daraja la II
Halmashauri Zilizohusika
- Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
- Halmashauri ya Wilaya ya Busega
- Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
Muhimu kwa Walioitwa Kazini
Waombaji wote waliofanikiwa wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal kupitia sehemu ya “My Applications” ili kupakua barua zao za ajira na kwenda kuripoti kwenye vituo walivyopangiwa kwa muda uliotajwa kwenye barua hizo.
Walioitwa kazini wanatakiwa kwenda kuripoti wakiwa na vyeti vyao halisi (Original Certificates) kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua ya ajira rasmi.
Kwa wale ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili, wanashauriwa kuendelea kuomba nafasi nyingine zitakazotangazwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Pakua Orodha Kamili ya Majina
Upsten Ajira Portal tunaendelea kukuletea taarifa sahihi na za haraka kuhusu ajira, matokeo ya usaili pamoja na waliitwa kazini Tanzania.
